Leo Mei 30, 2025 Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeadhimisha siku ya Wauguzi Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 ya Mwezi Mei Duniani kote.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Hospitali ya Manispaa ya Geita na mgeni rasmi akiwa Ndg. Yefred Myenzi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "Uuguzi Nguvu ya Mabadiliko"
Ndg. Myenzi akihutubia maadhimisho hayo, amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuikumbuka Manispaa ya Geita kutuletea watumishi wa kada ya afya 46 wakiwemo wauguzi pamoja na vifaa tiba.
Katika hotuba yake Ndg. Myenzi amewapongeza wauguzi kwa kusema kusema wameendelea kuonyesha moyo wa kipekee kwa namna wanavyojitoa katika kuifanya kazi yao kwa moyo wote
Amewapongeza pia kwa kusema anaridhishwa na utendaji kazi wa watumishi nakusema Geita Manispaa inaendelea kujitahidi kuhakikisha upatikanaji wa Dawa na vifaa tiba
Myenzi amesisitiza watumishi kuendelea kuipenda kazi yao na kuifanya bila kuchoka na amewakumbusha juu ya kiapo chao kuwa ni ahadi ya moyo dhamira na utu hivyo wanatakiwa kukiishi kiapo chao ili kuepuka kuondolewa kiapo hicho na kulinda misingi ya kitaaluma kwa kufuata miongozo ya matibabu
Pia amewataka kufuata miiko ya kazi kwa kuacha yale yasiyotakiwa kufanywa ikiwa ni pamoja na kutotoa dawa zisizofaa kwa wagonjwa pamoja na kuepuka kutoa au kupokea rushwa hii ikiambatana na kusimamia miiko yao ya kazi kama kutotoa siri za wagonjwa maana kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha ya Mgonjwa
Wakati huo huo, ameipongeza idara ya afya kwa kuondoa tatizo la watumishi wasio waadilifu, wanaotoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa kwani kufanya hivyo kutasaidia kulinda heshima ya kada ya afya
Na mwisho ameendelea kusisitiza watumishi kuendelea kuhifadhi vifaa na dawa ili kuepusha upotevu na hasara.
Maadhimisho haya hufanyika kila mwaka Mei 12, Duniani kote ikiwa ni kumbukumbu kwa muasisi wa huduma ya Uuguzi Florence Nightngale ambaye alikuwa Muitaliano aliyezaliwa mwaka 1871 na Kitaifa yamefanyika Mkoani Mara
Kwa mwaka huu 2025 maadhimisho ya siku ya Wauguzi Katika Manispaa ya Geita yameambatana na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwatembelea wagonjwa na kufanya matembezi ya amani na burudani mbalimbali.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa