Halmashauri ya Manispaa ya Geita imefanikiwa kupata Tuzo ya Halmashauri Bora katika uendeshaji wa shughuli za Michezo kwa mwaka 2024/2025.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kasim Majaliwa Kasim akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndiye aliyekabidhi Tuzo hiyo ambayo imetolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Ndg. Yefred Myenzi.
Tuzo hiyo imepokelewa leo tarehe 22 Aprili, 2025 na Bi Juliana Kimaro, Afisa Michezo katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita kwa niaba ya Mkurugenzi wa Minispaa
Bi. Juliana Kimaro, Afisa Michezo katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita akipokea tuzo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Minispaa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeandaa Kikao Kazi cha 15 cha Maafisa Utamaduni na Maafisa Michezo wa Nchi nzima kinachofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22-25 Aprili, 2025.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa