Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia iliyopo katika Manispaa ya Geita Mkoani humo ikiongozwa Mwakilishi kutoka Wizara ya katiba na Sheria Ndg. Moses Matiko imeendelea na shughuli ya kutembelea na kutoa elimu katika shule ya sekondari ya wasichana Geita pamoja na shule ya Sekondari Kalangalala ambapo jopo la Mawakili pamoja na Maafisa wametoa elimu pamoja na kusikiliza migogoro.
Wanafunzi pamoja na walimu wameipongeza serikali kwa jitihada walizozifanya katika kuthamini mchango wa wananchi huku wakimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mpango huu wa kutatua migogoro kupitia kampeni hii ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia inayozunguka katika kata mbalimbali .
Aidha Jopo la Mawakili pamoja na Maafisa wametembelea pia Kata ya Bungwangoko iliyopo Manispaa ya Geita ambapo wametatua migogoro mbalimbali ikiwemo migogoro ya Ardhi , Masuala ya Kifamilia pamoja na migogoro ya kisheria.
PICHA MBALIMBALI KATIKA MATUKIO
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa