• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Geita Town Council
Geita Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali Watu na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Miundombinu, Maendeleo vijijini na Mjini
      • Usimamizi taka na Usafi wa Mazingira
    • Vitengo
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Sheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uchimbaji Madini
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Elimu na Afya
      • Kamati ya Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu ya Maombi
    • Miongozo
    • Jarida la Halmashauri
    • Mkakati wa kuziwezesha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
  • Maeneo ya Uwekezaji

Elimu ya COVID-19 KULETA MABADILIKO KWENYE JAMII

Posted on: April 30th, 2020

Elimu Ya COID-19 Kujenga Uelewa Mkubwa Kwa Jamii

Mafunzo juu ya uelewa wa kina kuhusu Virusi vya COVID-19,namna inavyoambukiza na jinsi ya kujikinga yaliyotolewa na wataalam wa elimu ya Afya kwa Umma kutoka Halmashauri za Wilaya na Geita mji kwenda kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii yamebainishwa kuleta matokeo chanya kwa wananchi wa Wilaya ya Geita.

Hilo limebainishwa na washiriki wa mafunzo ya siku mbili kuhusu namna ya kujilinda na maambukizi ya Virusi vya Corona yaliyofanyika Tarehe 22-23/04/2020 katika Chuo cha Uuguzi na Ukunga Geita Mjini kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kutoka katika mitaa na Kata mbalimbali za Wilaya ya Geita, Mafunzo ambayo yamefadhiliwa na Shirika la Plan International.

Bi. Suzana Kazige Sindano ambaye ni Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii kutoka Kijiji cha Chibingo Halmashauri ya Wilaya ya Geita ametoa wito kwa washiriki wenzake kutumia elimu waliyoipata kufikisha ujumbe toshelezi kwa jamii inayowazunguka ili waelewe kiundani juu ya mlipuko wa Virusi vya Corona. Pia amelishukuru Shirika la Plan kwa kuwaletea wataalam wa Afya kuwapatia elimu juu ya ugonjwa huo ulioitikisa dunia.

Kwa upande wake Ndg. Nathanael Kagoma, Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii kutoka mtaa wa Lutozo Halmashauri ya Wlaya ya  Geita amesema jamii yake  bado haijaelewa kiundani kuhusu namna ya kujilinda au kujikinga na maambukizi ya virusi vya COVID-19 . Elimu waliyoipata kutoka kwa wataalam wa afya imewapa mbinu mpya za ufundishaji utakaorahisisha jamii yake kupambana kikamilifu katika kujikinga na virusi vya COVID-19.

“Mara kwa mara nimekuwa nikisikia maelekezo ya namna ya kuepukana na maambukizi ya Virusi vya Corona kwa kusikiliza matangazo yanayorushwa na kituo cha Redio ya Storm FM, lakini leo nalishukuru sana Shirika la Plan kwa kutambua umuhimu wetu na kutuwezesha kupata elimu ya ana kwa ana pia kujifunza kwa vitendo jinsi ya kunawa mikono, kuvaa barakoa,kutumia vitakasa mikono na mengineyo ambayo yatawawezesha kufikisha ujumbe halisi kuhusu Virusi vya COVID-19  kwa jamii wanayoihudumia”. Alisema Bi. Anna Kassala, Mhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kutoka Kata ya Kanyala Halmashauri ya Mji Geita.

Ndugu Selestine Dominick Mafunganya, Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii kutoka Mtaa wa Kaduda Wilayani Geita amedhihirisha furaha yake kwa kuwashukuru Plan International kwa kuwakutanisha wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kutoka katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Geita ambapo baada ya mafunzo watapata fursa ya kubadilishana mawazo juu ya mbinu watakazozitumia kufikisha elimu ya COVID-19 kwa jamii. Kadhalika ameeleza kuwa atashirikiana na uongozi wa mtaa wake kufikisha elimu katika maeneo ya masoko, makanisani, msikitini, vikao vya Kamati za Mitaa na Kata ili watu wengi waweze kunufaika na elimu juu ya mapambano ya ugonjwa wa Corona.

Shirika la Plan International limewezesha mafunzo kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kutoka mitaa na  vijiji mbalimbali ndani ya Wilaya ya Geita ikiwa ni jitihada za shirika hilo kuhakikisha linashirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona ambao unaendelea kuutikisa ulimwengu mzima.



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA GEITA June 03, 2025
  • TANGAZO KUHUSU FURSA ZA MIKOPO YA ASILIMIA 10 May 27, 2025
  • Zaidi

Habari Mpya

  • MKUTANO MAALUMU WA BARAZA WA KUJADILI MAJIBU YA HOJA NA MAPENDEKEZO YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

    June 11, 2025
  • BILIONI 19.1 KUTEKELEZA UJENZI KITUO KIKUU CHA MABASI MANISPAA YA GEITA

    June 06, 2025
  • WATUMISHI GEITA MANISPAA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA

    June 05, 2025
  • WATUMISHI WA MANISPAA YA GEITA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA MITANDAO YA KIJAMII YENYE TAARIFA ZA UPOTOSHAJI

    June 04, 2025
  • Zaidi

Video

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA ITIKADI ZA KISIASA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Mfumo wa Watumishi kujihudumia
  • Applications Forms
  • Acts
  • Taarifa za Huduma za Afya
  • Mfumo wa Kupata Leseni za Biashara ( Mfumo wa Tausi)
  • Barua pepe za watumishi
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Taarifa za Mapato

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Geita Tanzania

    Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita

    Namba ya Simu: 0282520437

    Mobile:

    Barua pepe: td@geitatc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa