Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mheshimiwa Hashimu Abdalah Komba, amekutana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea pamoja na viongozi wa Kata ya Nditi na kutoa ushauri mahsusi kuhusu namna ya kuimarisha uwekezaji wa madini.
Katika ushauri wake, Mhe. Komba alisisitiza umuhimu wa kutowasambaratisha wachimbaji wadogo na badala yake waendelezwe kwa kutengewa eneo rasmi kwani wachimbaji hawa ni kichocheo kikubwa cha mageuzi ya kiuchumi kwa jamii na kipato cha mtu mmoja mmoja.
Pia,alishauti kuibua miradi ya kimkakati itayokamilika moja kwa moja na sio kuanzishwa nusunusu kwa kuwatumia wawekezaji ambao watawekeza katika kuchimba madini ya nickel, graphite, kopa, dhahabu na mengine yanayopatikana Nachingwea.
Mheshimiwa Komba alishauri kuanzishwa kwa chuo kidogo cha kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa migodini ili kuwawezesha wananchi wa Nachingwea kupata fursa ya kuajiliwa kama ilivyo kwa Geita, kwa kushirikiana na VETA au kwa msaada wa wawekezaji, ili kuongeza ujuzi wa vijana katika sekta hiyo.
Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ndugu Lington Nzunda ametoa shukrani za dhati kwa mheshimiwa Komba na Wilaya ya Geita kwa ushauri na elimu waliyojifunza kuhusu usimamizi mzuri wa migodi kwani Nachingwea inakwenda kupata wawekezaji wakubwa hivi karibuni katika mgodi uliopo kijiji cha Mditi.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa