Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba leo tarehe 20 Juni, 2024 amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Kata ya Mgusu iliyopo katika Halmashauri ya Mji Geita ikiwa ni sehemu ya usimamiaji wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujitambulisha kwa Wananchi wa Kata hiyo kutokana na kuhamishiwa kwake katika Wilaya hii akitokea Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Ziara hiyo ya Mhe. Komba imehusisha viongozi mbalimbali wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Kata, Kamati ya Usalama ya Wilaya ikiongozwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya, Afisa Tarafa ya Geita, pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Geita aliyeambatana na Wakuu wa Divisheni na Vitengo (Wataalamu) mbalimbali.
Taasisi zingine zikizoshuriki katika ziara hii ni pamoja TARURA, TANESCO, GEUWASA na Mgodi wa Dhahabu wa GGM
Miradi iliyotembelewa na Mhe. Komba ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya polisi, kituo cha afya Mgusu, ujezi wa zahanati ya Mtaa wa Manga, ujenzi wa darasa moja katika shule ya Sekondari Mgusu na ujenzi wa daraja la Mto Mtakuja lililopo katika Mtaa wa Nyakabale.
Akiongea wakati wa ziara hiyo Mhe. Komba amesema kuwa Miradi yenye changamoto ifanyiwe kazi na miradi ambayo inaanza na ile inayoendelea itekelezwa kwa viwango vya juu. Pia kuhakikisha miradi ya zamani na mipya inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa ili Wananchi wapate huduma stahiki.
Aidha, DC Komba imeipongeza Serikali chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi mingi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ili kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa