Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba leo tarehe 22 Aprili, 2025 ameongoza kikao maalum cha kwanza cha wadau wa mazingira kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika viwanja vya maonyesho Bombambili
kikao hiki maalum cha wadau wa Mazingira kimekuwa na lengo kuu la kujadili masuala ya usafi wa mazingira, udhibiti wa taka na upendezeshaji wa maeneo ya manispaa ya Geita.
Kikao hicho kiliambatana na uandaaji wa mpango kazi wa utekelezaji wa Mradi usafi katika Halmashauri ya Manispaa Geita na kikao hiko kimejumuisha wadau mbalimbali kama vile; Waheshimwa madiwani, kamati ya ulinzi na usalama wakiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya, viongozi wa dini, wakuu wa idara na vitengo kutoka Manispaa na taasisi zingine zilipo ndani ya Manispaa.
Wadau wengine ni pamoja na Viongozi wa Chama Ngazi ya wilaya hadi kata, wajumbe wa Serikali za Mitaa, Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa, Wafanyabiashara, wawakilishi wa vikundi mbalimbali vya mazingira na wadau wengine mbalimbali
Hata hivyo, wadau wameweka mbinu na mikakati bora ya kuimarisha utekelezaji wa Mradi wa ukoreshaji wa Mazingira na uhifadhi bora wa taka katika Manispaa ya Geita yenye azma ya kuwa na Manispaa safi, salama na yenye kuvutia
Akifunga kikao hicho Mhe. komba amesema kuwa kutakuwa na kampeni maalumu yenye lugha ya kisukuma Hyagulaga Geita Geita ikiwa na maana Safisha Geita ambayo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 26 Aprili, 2025 wakati maadhimisho wa sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Geita.
Akifafanua zaidi juu ya kampeni hiyo Mh. Komba amesema kuwa kampeni hiyo itaanza rasmi tarehe 01 Mei, 2025 na itakuwa inaambatana na utoaji wa zawadi kila baada ya miezi mitatu kama motisha katika makundi mbalimbali kama vile washindi watatu wa kwanza na washindi wa tatu wa mwisho kwa ngazi ya mtaa, nyumba, taasisi n.k, balozi wa mazingira, wajasiriamali na wafanyabiashara wenye kutunza mazingira sehemu zao za biashara n.k lengo kuu ya kampeni hii ni kuhakikisha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Geita inakuwa safi, salama na yenye kuvutia.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa