Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba, amelaani vikali mauaji ya mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwatulole uliopo katika Kata ya Buhalahala Ndg. Noel Ndasa yaliyotokea tarehe 23 June 2024 majira ya nyumbani kwake Mwatulole
Mhe. Komba amesema hayo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nyaseke kilichopo katika katika kata ya Bulela.
Amethibitisha kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa Serikali ya Mtaa na watu wasiofahamika waliovamia nyumbani kwa marehemu na kumshambulia kwa mapanga na kusababisha kifo chake. Aidha, Mhe. Komba amelitaka jeshi la polisi kuendelea na uchunguzi wa kina na hatimaye wahusika wa tukio hilo wafikishwe katika vyombo vya sheria
Wakati huo huo, Mhe. Komba amelaani mauwaji ya watu wenye mahitaji maalum hasa wenye ulemavu wa ngozi (Albino) kwa kile kinachohusishwa na imani za kishirikina na ameitaka jamii kutofumbia macho matendo maovu bali watoe taarifa katika vyombo vya sheria
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Komba amekuwa kwenye ziara Kata ya Bulela ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea Kata zote za Halmashauri ya Mji Geita iliyoanza tarehe 18 June, 2024 kwa ajili ya kujitambulisha, kuijua Halmashauri ya Mji wa Geita, Kutembelea na kukagua miradi iliyokwama ili iweze kukamilishwa na kuanza kutoa huduma lakini pia kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majibu.
Ziara hiyo ya Mhe. Komba imehusisha viongozi mbalimbali wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Kata, Kamati ya Usalama ya Wilaya ikiongozwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya, Afisa Tarafa ya Geita, pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Geita aliyeambatana na Wakuu wa Divisheni na Vitengo (Wataalamu) mbalimbali.
Taasisi zingine zilizoshiriki katika ziara hii ni pamoja TARURA, TANESCO, GEUWASA na Mgodi wa Dhahabu wa GGM
Akiwa katika ziara hiyo, Mhe. Komba ametembelea miradi mbalimbali muhimu ikiwemo ya afya, maji, barabara na kusikiliza kero zao na kuzitafutia majibu kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nyaseke kilichopo katika katika kata ya Bulela
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa