Mhe. Komba ametoa ahadi hiyo baada ya kukagua ujenzi wa Soko la Mtaa wa Compound ambao unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai, 2024.
DC Komba leo amekuwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Kata ya Mtakuja ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kuzitembelea Kata zote kumi na tatu (13) zilizopo katika Halmashauri ya Mji Geita
Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya wakipokea zawadi toka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtakuja
Akiwa katika Kata hii ya Mtakuja Mhe. Komba ametembelea miradi ifuatayo; ujenzi wa soko la Mtaa wa Compound, shule mpya ya sekondari Mtakuja iliyopo katika Mtaa wa Nyamalembo, ujenzi wa Zahanati ya Bihengule na ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Mbabani iliyopo katika mtaa wa Mbabani ambapo shule hii ndiyo shule itakayokuwa ya amali (Shule ya Ufundi) katika Halmashauri ya Mji Geita
Akibainisha hilo Mkurugenzi wa Mji Ndg. Myenzi amesema wataalam kutoka Wizarani walishafika kubainisha eneo hilo na waliona linafaa hivyo tunachosubiria ni maelekezo ya kiserikali ilio utekelezaji wa mradi uendelee.
Aidha Mhe. Komba wakati akiwa anatembelea miradi katika Mtaa wa Mbabani aliweza kutembelea ujenzi madarasa katika shule ya msingi Mbabani yanayojengwa kupitia Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) chini ya mpango wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) na kuwataka wakadarasi wote waliopewa mikataba chini ya CSR kuhakikisha wanakamilisha kazi zao kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa
Katika salamu zake kwa wananchi Diwani wa Kata ya Mtakuja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita, Mhe. Costastine Morandi Mtani amshukuru sana Mhe. Rais kuleta umeme katika Mtaa wa Mbabani Pamoja na kuleta miradi mingi katika Halmashauri ya Mji kwa ujumla.
Aidha, baada ya ziara hiyo Mhe. Komba alifanya mkutano wa hadhara katika Mtaa wa Mpomvu ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Komba akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mtakuja
Ziara hiyo ya Mhe. Komba imehusisha viongozi mbalimbali wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Kata, Kamati ya Usalama ya Wilaya ikiongozwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya, Afisa Tarafa ya Geita, pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Geita aliyeambatana na Wakuu wa Divisheni na Vitengo (Wataalamu) mbalimbali.
Taasisi zingine zikizoshuriki katika ziara hii ni pamoja TARURA, TANESCO, GEUWASA na Mgodi wa Dhahabu wa GGM
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa