Nyamhongolo, Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim A. Komba, amefungua rasmi Maonesho ya Kilimo na Mifugo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Nyamhongolo, Jijini Mwanza, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ndugu Martine Shigela.
Katika hotuba yake, Mhe. Komba amewahimiza wakulima na wananchi wote wanaotembelea maonesho hayo kuhakikisha wanatembelea mabanda mbalimbali ili kujifunza mbinu za kisasa za kilimo, ufugaji, usindikaji na matumizi ya teknolojia bunifu katika sekta ya kilimo.
“Nanenane ni jukwaa muhimu sana ambalo huwakutanisha wadau wakubwa wa kilimo, wataalamu, wajasiriamali na wakulima wadogo kwa lengo la kubadilishana maarifa,” amesema Mhe. Komba.
Aidha, ametoa rai kwa makampuni na taasisi mbalimbali kuendelea kujitokeza kudhamini na kushiriki katika maonesho hayo ambayo yanabeba dira ya maendeleo ya kilimo cha kisasa.
Katika hitimisho la hotuba yake, Mhe. Komba aliwakumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura litakalofanyika mwezi Oktoba, kama sehemu ya kuimarisha demokrasia ya nchi.
Kwa upande wao, Maafisa na wataalamu wa kilimo kutoka Manispaa ya Geita wameeleza dhamira yao ya kuendelea kushiriki kikamilifu katika maonesho ya Nanenane kwa lengo la kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji, ili kuongeza tija na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Taifa.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa