Timu ya wataalamu kutoka Dawati la Kusikiliza na Kutatua Malalamiko ya Wananchi, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, imefanya ziara ya utalii wa ndani katika Kisiwa cha Rubondo kilichopo ndani ya Wilaya ya Geita, ikiwa ni sehemu ya kujifunza, kuburudika na kujionea vivutio vya asili vinavyopatikana ndani ya Mkoa wa Geita.
Ziara hiyo imeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba, akiambatana na Katibu Tawala wa Wilaya, Bi. Lucy Beda pamoja na wataalamu wengine wa dawati hilo.
Katika ziara hiyo, washiriki walipata fursa ya kutembelea maeneo yenye vivutio kama vile wanyama wa porini, ndege wa aina mbalimbali, mamba na mandhari ya kuvutia, yote hayo yakionyesha utajiri wa vivutio vya kipekee vilivyopo Rubondo.
Bi. Lucy Beda, Katibu Tawala wa Wilaya, alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwawezesha kushiriki, akisema
“Tumepata fursa ya kujifunza, kufurahia, na kuona umuhimu wa kukuza utalii wa ndani kwa vitendo
Mhe. Komba, kwa upande wake, aliipongeza Menejimenti ya Rubondo kwa mapokezi bora na namna wanavyosimamia utalii.
“Tutakuwa mabalozi wa kutangaza utalii wetu. Rubondo ni hazina ya kipekee ya utalii inayopaswa kutambulika zaidi,” alisema Mhe. Komba.
Aidha, amesisitiza kuwa ziara kama hizi ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya *Tanzania The Royal Tour* inayoendeshwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kukuza utalii wa ndani na kuitangaza Tanzania kimataifa.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa