Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita Mhe. Costantine Morandi Mtani Leo tarehe 30 Januari, 2025 ameongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani, na Baraza hilo limeridhia kupitisha rasimu ya bajeti ya Shilingi Bilioni 68,393,812,906.00 kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Bajeti hii ina ongezeko la 13.2% zaidi ya ile ya mwaka wa fedha 2024/2025 Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Halmshauri wa EPZ uliopo katika Viwanja vya Maonesho.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita Mhe. Costantine Morandi Mtani
Kati ya bajeti hiyo shilingi bilioni 47,547,078,004.00 sawa na 69.6% ni ruzuku kutoka Serikali Kuu na Shilingi bilioni 20,846,734,902.00 sawa na 30.4% zitatokana na mapato ya ndani ambayo ni ongezeko la asilimia 4.2 kutoka bajeti ya mwaka 2024/2025 kwa Shilingi bilioni 19,965,455,000.00
Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili na kupitisha rasimu ya bajeti hiyo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita Mhe. Costantine Morandi Mtani amesema bajeti hiyo imezingatia mapendezo yote muhimu ya waheshimiwa madiwani na hivyo itakwenda kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Geita wakifuatilia Mkutano wa Baraza hilo
Akiwasilisha rasimu ya bajeti hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Ndg. Samson Ndaro amesema Halmashauri inakadiria kupokea na kutumia jumla ya shilingi 68,393,812,906.00 kutoka katika vyanzo mbalimbali.
Ndg. Ndaro ameongezea kusema vyanzo hivyo ni mapato ya ndani shilingi bilioni 20,846,734,902.00, matumizi mengineyo (Ruzuku ya Serikali) shilingi bilioni 1,031,607,000.00, Mishahara (Ruzuku ya Serikali) shilingi bilioni 32,286,649,150.00, miradi: fedha za ndani (Ruzuku) shilingi bilioni 4,219,164,414.00, miradi: fedha za nje (Wahisani) 4,634,413,0000.00, CSR Shilingi bilioni 5,025,244,440.00 na michango ya wananchi na wadau wengine wa maendeleo shilingi milioni 350,000,000.00
Aidha, Ndg. Ndaro amesema vipaumbele vya bajeti hiyo ni kuongeza mapato ya ndani kutoka bilioni 19,965,455,000.00 ya sasa hadi bilioni 20,846,734,902.00, ili kuimarisha shughuli za utawala bora, Kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya, Uimarishaji wa usafi wa mazingira, Kuboresha miundombinu ya shule za Msingi, Uwezeshaji wananchi kiuchumi, Ukamilishaji wa miradi viporo, Umilikishaji wa maeneo ya umma.
Aidha Waheshimiwa Madiwani wameonesha kuwa na Imani na maono chanya katika maandalizi ya mipango na bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwemo Baraza la wafanyakazi, kamati ya ukimwi, kamati ya elimu, kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira, kamati ya fedha, Utawala na mipango.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia Baraza la Madiwani
Hata hivyo katika Baraza hilo la kupitisha rasimu ya bajeti Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita Ndg. Yefred Myenzi amewapongeza Waheshimiwa Madiwani wa kata zote kwa kuwa wafuatiliaji wa miradi ya maendeleo na michango yao katika kuendeleza Halmashauri, Pia ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za kuendeleza miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya maji, barabara, umeme, ujenzi wa shule na vituo vya Afya.
Ndg. Yefred Myenzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita akichangia hoja katika Baraza hilo
Naye, Katibu wa Wilaya wa Chama cha Mapinduzi CCM, Ndg. CDE. Michael Msuya, amewapongeza madiwani na wataalamu kuwa na umoja katika kuijenga Manispaa ya Geita, amewataka pia kushirikiana na viongozi wa ngazi ya Mitaa na Vijiji katika ukusanyaji wa mapato na waisimamie ili iweze kuwanufaisha wao na wananchi kwa ujumla.
Katibu wa Wilaya wa Chama cha Mapinduzi CCM, Ndg. CDE. Michael Msuya akichangia hoja katika Baraza hilo
Uandaji wa Mpango na rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26, umeandaliwa kwa mujibu wa Kifungu na. 21 cha sheria ya bajeti, sura 439 na kanuni zake za mwaka 2015. Maandalizi ya mpango huu wa bajeti yamezingatia ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mpango wa tatu wa maendeleo ya Taifa wa miaka mtano 2021/22 - 2025/26, malenzo ya maendeleo endelevu 2030 na maelekezo mahsusi ya serikali.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa