Asubuhi ya leo, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mbaruku, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, ametembelea vituo vitatu vya uboreshaji wa taarifa za wapiga kura katika maeneo mbalimbali. Vituo alivyotembelea ni pamoja na:
Katika ziara hiyo, Mh. Jaji Mbaruku ameridhishwa na mwitikio mzuri wa wananchi ambao wamejitokeza kwa wingi kuboresha taarifa zao na kujiandikisha kama wapiga kura. Amepongeza wananchi kwa kuonyesha uzalendo na uelewa wa haki yao ya kidemokrasia.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi wote ambao bado hawajafanya hivyo, kuhakikisha wanatumia siku hizi zilizobaki saba kujiandikisha au kuboresha taarifa zao. Amesisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza, hivyo ni muhimu kutumia nafasi hii kikamilifu.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa