• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Geita Town Council
Geita Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali Watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Nyuki na Misitu
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uchimbaji Madini
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Elimu na Afya
      • Kamati ya Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu ya Maombi
    • Miongozo
    • Jarida la Halmashauri
    • Mkakati wa kuziwezesha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Wananchi Watakiwa Kupinga Ukatili

Posted on: December 11th, 2020

Wananchi Watakiwa Kupinga Vitendo Vya Kikatili

Wananchi wa Kata ya Mgusu na Halmashauri ya Mji wa Geita kwa ujumla wameaswa kuhakikisha kuwa wanapinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea katika maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tarafa wa Geita Ndugu Innocent Mabiki alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Geita wakati wa Maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizofanyika hivi karibuni katika Kata ya Mgusu.

Ndg. Mabiki ameeleza kuwa kulingana na taarifa zinazotolewa na Idara ya Maendeleo ya jamii katika kata ya Mgusu bado kuna viashiria vinavyoonyesha uwepo wa matukio mbalimbali ya ukatili wa kijinsia kwa pande zote mbili  na ili kukomesha suala hilo wananchi wanatakiwa kukemea vitendo hivyo na kutoa taarifa kwenye mamlaka za kiserikali pindi vitendo hivyo vinapotendeka.

Afisa Tarafa wa Geita pia ameishauri Idara ya Maendeleo Halmashauri ya mji Geita kujitahidi kutoa elimu / warsha au makongamano ya mara kwa mara kwenye jamii ili wananchi waweze kuelewa athari na  kuepuka kutendeana ukatili  wa kijinsia.

Mtendaji wa Kata ya Mgusu Victor Bashingwa amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo wakati wa utatuzi wa kesi zinazohusisha matendo ya kikatili ni tabia ya upande wa walalamikaji hususan wanawake kukatisha muendelezo wa mashtaka kwa kuomba waume zao wasamehewe kwa ukatili walioufanya kwa wake zao na watoto na kuzifanya kesi hizo kushindwa kufikia hatua za kisheria.

Kwa upande wake Mratibu wa dawati la Maendeleo ya jinsia Halmashauri ya Mji Geita Bi. Saga Mtaki amesema kuwa ofisi yake hupokea wanawake na watoto ambao huathirika na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikilinganishwa na wanaume. Ukatili huo ni kama vile ukatili wa kimwili, kingono, kisaikolojia na ukatili wa kiuchumi.  Ambapo kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Novemba 2020 wanaume 43, wanawake 215 na watoto 16 wamejitokeza kuleta taarifa na malalamiko.



Matangazo

  • Fomu za Kuijiunga Kidato cha Kwanza Shule ya Sekndari Nyankumbu na Geita December 29, 2020
  • TANGAZO LA KODI YA MAJENGO April 20, 2018
  • TANGAZO LA WAMILIKI WA VIWANJA VILIVYOSHINDWA KUENDELEZWA BOMBAMBILI NA MAGOGO May 28, 2018
  • TAARIFA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI YA HESABU ZA KUISHIA TAREHE 30 JUNI 2017 June 29, 2018
  • Zaidi

Habari Mpya

  • Mapato ya Ndani Kujenga Miradi ya Kimkakati

    March 04, 2021
  • Wananchi Wakumbushwa Kulipa Kodi Kwa Muda

    March 02, 2021
  • Geita Mji Yajipanga Kuepuka Mrundikano wa Wanafunzi

    February 15, 2021
  • Wananchi Watakiwa Kupinga Ukatili

    December 11, 2020
  • Zaidi

Video

Bombambili Bomba ndani ya Miaka 5 ya JPM
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Applications Forms
  • Acts
  • Barua pepe za watumishi
  • Taarifa za Huduma za Afya
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Taarifa za Mapato

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Geita Tanzania

    Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita

    Namba ya Simu: 0282520437

    Mobile:

    Barua pepe: td@geitatc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa