IDARA YA ELIMU SEKONDARI
MAJUKUMU YA ELIMU SEKONDARI:
1.Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Sheria na Kanuni zinazoongoza utoaji wa elimu ya sekondari;
2.Kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu masuala yote ya elimu ya sekondari;
3.Kusimamia upanuzi wa elimu ya sekondari katika Halmashauri;
4.Kusimamia haki na maslahi ya walimu na watumishi wengine wa ngazi ya elimu ya sekondari katika Halmashauri;
5.Kuratibu na kusimamia mitihani ya kitaifa inayoendeshwa kwa shule za sekondari katika Halmashauri;
6.Kusimamia na kudhibiti akaunti ya elimu ya sekondari na kuhakikisha kuwa fedha za elimu ya sekondari zinatumika kama ilivyokusudiwa;
7.Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu ya sekondari kila mwaka;
8.Kufuatilia na kutathmini maendeleo ya elimu ya sekondari katika Halmashauri;
9.Kuhimiza shule zote za sekondari kuinua ubora wa mazingira ya kujifunzia na kufundishia ikiwa ni pamoja na kujenga madarasa, nyumba za walimu na vyoo;
10.Kuhimiza udhibiti wa nidhamu ya walimu na wanafunzi wa shule za sekondari katika Halmashauri;
11.Kufuatilia utekelezaji wa taarifa za Ukaguzi wa Shule za Sekondari;
12.Kusimamia maendeleo ya taaluma na michezo ya shule za sekondari katika Halmashauri;
13.Kuratibu, kukusanya na kuchambua takwimu za elimu ya sekondari katika Halmashauri;
14.Kuhakikisha walimu wa shule za sekondari wanapangwa katika Halmashauri kwa kuzingati ikama inayokubalika; na
15.Kufanya kazi nyingine kama utakavyoelekezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri.
Kupata idadi ya shule zote bonyeza hapa.
WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI MJI GEITA.xls
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa