Mradi mkubwa wa uchimbaji wa visima 150 kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya kilimo katika mkoa wa Geita. Visima hivyo vitachimbwa katika Halmashauri zote za Mkoa huo, na lengo kuu ni kuwawezesha wakulima kulima kwa mwaka mzima bila kutegemea mvua.
Uzinduzi rasmi wa mradi huo umefanyika tarehe 16 Oktoba, 2025 katika Kijiji cha Mwilima, Kata ya Kanyala – Manispaa ya Geita, ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin. Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mhe. Martin amesema mradi huu ni sehemu ya jitihada za serikali katika kuinua sekta ya kilimo na kuwaondoa wakulima kwenye kilimo cha mazoea kuelekea kilimo chenye tija na kibiashara.
Kwa Kata ya Kanyala pekee, visima hivyo vitahudumia zaidi ya ekari 1,400, hatua inayotarajiwa kuongeza uzalishaji wa mazao na kipato kwa wananchi. Mradi huu unalenga sio tu kuongeza uzalishaji bali pia kuboresha maisha ya wakulima na kuchochea uchumi wa mkoa.
Mkoa wa Geita unaendelea kuwa mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia usimamizi thabiti wa viongozi wake na ushirikiano wa karibu na wananchi.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa