Hayo yamesemwa leo tarehe 22 Novemba, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba wakati wa ziara ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kata ya Nyanguku.
”Tulinde amani na utulivu wa Nyanguku yetu, hatuna Nyanguku nyingine zaidi ya hii, Tulinde amani na utulivu wa Geita yetu, hatuna Geita nyingine zaidi ya hii” amesema Mhe. Komba
Pia, Mhe. Komba akiwahutubia wananchi wa Mtaa wa Kakonda amewaagiza Maafisa Kata wote wa Halmashuri ya Manispaa ya Geita kuhakikisha wanahuisha Kamati za Ulinzi na Usalama zikae vikao vyake na kutoa mrejesho katika mamlaka husika na kuwatambua Polisi Jamii (Sungusungu) wote na kushirikishwa katika swala la ulinzi na usalama.
Akijibu kero ya wizi wa Mifugo, Mhe. Komba amekemea tabia hiyo kwani inarudisha nyuma maendeleo ya mtu na Taifa kwa ujumla na alitumia wasaa huo kuendesha kura ya siri kwa wananchi kupiga kura kuwabaini wezi wa mifugo kwa majina ili kuwachunguza na kuwachukulia hatua zaidi pindi watakapopatikana na hatia ya makosa ya wizi wa mifugo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Komba aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita na Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Geita na amefanya mkutano wa hadhara katika Mitaa mitatu ambayo ni Nyanguku, Nyakato na Kakonda.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa