Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela leo Novemba 11, 2025 amekagua ujenzi wa mradi wa barabara ya kiwango cha lami (Mkolani - Mwatulole, Nyankumbu - Kivukoni) sehemu ya Mwatulole yenye urefu wa kilomita 17 na kumtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kufanya kazi kwa haraka ili mradi uweze kukamilika kwa muda uliobakia ili kuwanufaisha wananchi kama lilivyo kusudi la Serikali.
Mhe. Shigela ametoa agizo hilo baada ya kufanya ukaguzi wa mradi huo ambao unafadhiliwa na benki ya dunia kwa gharama za kitanzania Bilioni 22.2 na kuongeza kuwa barabara hiyo ina umuhimu mkubwa hasa katika kuimarisha shughuli za kiuchumi na kijamii.
Mradi huu wa barabara unajulikana kama Uboreshaji kwa Kiwango cha Lami Barabara ya Mkolani - Mwatulole, Nyankumbu - Kivukoni, Nguzombili - Samandito inayounganisha Emma - Mamakengele - Mwabasabi na Mwatulole - Mshinde Twiga yenye jumla ya kilomita 17 na unafadhiliwa na benki ya dunia kwa gharama za kitanzania 22,232,794.212/= na unatarajiwa kukamilika februari 2026.
Kwa sasa mradi huu ushafikisha asilimia 61 na Mkandarasi wa mradi huu ni Sichuan Road and Bridge (Group) Corporation LTD na Msimamizi (Mhandisi Mshauri) Luptan Consults LTD kwa Ushirikiano na Safi Consultants LTD wote wakitokea Dar es Salaam
Wakati huohuo, Mhe. Shigela ametambelea na kukagua ujenzi wa shule ya msingi Nyantindili iliyopo katika Mtaa wa Elimu katika Kata ya Nyankumbu, ambapo amewapongeza wananchi wa Nyankumbu kwa kuonesha jitihada zao za kujenga msingi wa vyumba vya madara na amewaahidi kuwachangia tofali elfu mbili (2,000) huku ofisi ya Mkuu wa wilaya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba ikiahidi mifuko 50 ya saruji.
Ujenzi wa shule hii ulianza rasmi tarehe 03 Septemba, 2025 kwa hatua za uchimbaji wa wa msingi na ununuzi wa vifaa vya ujenzi. Utekelezaji wa mradi huu umefanyika kwa kujenga vyumba vitano vya madarasa, ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa na ujenzi wa matundu sita ya choo, ambapo vyumba vyote saba vya madarasa vipo katika hatua ya uwekaji wa mifumo ya umeme huku matundu sita ya choo yapo katika hatua ya upigaji ripu.
Ujenzi wa shule hii hadi sasa umepokea fedha kiasi cha 163,600,000/= ikiwa mradi wa Boost 88,600,000/=, mapato ya ndani 50,000,000/= na serikali kuu 25,000,000/= na kiasi kilichotumika hadi sasa ni 158,018,000/= ikiwa mradi wa Boost 86,075,000/=, mapato ya ndani 49,327,500/= na serikali kuu 2,384,500/= na kiasi kilichobakia ni shilingi 5,582,000 ambacho kinaweza kukamilishia hatua zilizopakia bila changamoto yoyote.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita (RPC), Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Safia Jongo amewataka wazazi na walezi kuwa na malezi mazuri kwa watoto ili kuwa na vijana wa kesho walio wazalendo na wenye maadili.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa