Tarehe 26 Septemba 2025, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mheshimiwa Hashim A. Komba, amehitimisha rasmi ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita. Ziara hiyo maalum ililenga kutembelea na kukagua vikundi vya wajasiriamali vilivyonufaika na mikopo ya Asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa mujibu wa sheria.
Ziara hiyo ambayo aliipa jina la “4-4-2 Tour”, ilikamilika katika Kata ya Kalangalala, kwenye Ukumbi wa GEDECO, ambako Mheshimiwa Komba alikutana na vikundi vyote vilivyopata mikopo hiyo. Alitoa ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi sahihi ya mikopo, akisisitiza umuhimu wa kutumia fursa hiyo kwa maendeleo endelevu.
Katika hotuba yake, Mkuu wa Wilaya aliwahimiza wanavikundi kuepuka mikopo isiyo na tija maarufu kama “mikopo umiza/chefuchefu”, ambayo mara nyingi imekuwa chanzo cha matatizo kwa wajasiriamali wadogo. Aidha, alisisitiza kuhusu umuhimu wa kufanya marejesho kwa wakati, ili kuhakikisha kuwa wananchi wengine wengi zaidi wananufaika na mfuko huo wa mikopo kupitia Halmashauri.
Mheshimiwa Komba aliendelea kuhamasisha vikundi kuimarisha uzalishaji, kushirikiana na kutafuta masoko ya bidhaa zao, huku akiweka wazi kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wajasiriamali wote wanaochukua hatua za kuleta maendeleo kwa vitendo.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa