Oktoba 29, 2025 - Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba, leo ameshiriki zoezi la kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na kueleza kufurahishwa kwake na mwenendo mzima wa zoezi hilo, hususan utulivu na maandalizi mazuri yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura, Mhe. Komba ameipongeza Tume kwa mpangilio bora wa vituo vya kupigia kura, maandalizi ya vifaa, pamoja na usimamizi mzuri unaowezesha wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia kwa amani na utulivu.
“Nimefurahishwa sana na jinsi zoezi linavyoendelea. Vituo vimefunguliwa kwa wakati, wananchi wanafuata taratibu bila msongamano, na hali ni shwari kabisa. Nawapongeza wasimamizi wa uchaguzi na Tume kwa kazi nzuri,” alisema Komba
Aidha, Mhe. Komba amewahimiza wananchi wote wa Geita na maeneo mengine nchini kuendelea kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kupigia kura, akisisitiza kuwa kura ni haki ya msingi ya kila raia katika kuamua mustakabali wa taifa,
Zoezi la upigaji kura linaendelea nchi nzima kwa amani huku viongozi mbalimbali wakihamasisha ushiriki wa wananchi ili kuhakikisha kuwa sauti ya kila Mtanzania inasikika kupitia sanduku la kura.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa