Leo, 10 Oktoba 2025 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Ndugu Yefred Myenzi, amegawa kompyuta kwa Watendaji wa Kata nane (8) katika zoezi linalolenga kuboresha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi.
Zoezi hilo ni sehemu ya jitihada endelevu za Halmashauri kuwawezesha watumishi wa ngazi ya jamii kwa kuwapatia vifaa vya kisasa vinavyowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, hasa katika matumizi ya mifumo ya FFARS na uratibu wa utoaji wa mikopo ya 10% kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Akizungumza kwa niaba ya Watendaji waliopokea vifaa hivyo, Ndugu Victor, WEO kutoka Kata ya Kasamwa, amemshukuru Mkurugenzi kwa uamuzi huo na ameahidi kuwa vifaa hivyo vitatumika kwa umakini na vitatunzwa ili vidumu na kutumika kwa manufaa ya wananchi.
Zoezi la ugawaji limefanyika katika Makao Makuu ya Halmashauri, Magogo – Kata ya Bombambili, Geita.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa