Tarehe 2 Desemba 2025, Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeandika historia mpya baada ya Diwani wa Kata ya Bombambili, Mhe. Leonard Bugomola Kiganga, kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo.
Uchaguzi huo umefanyika katika kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa EPZ Bombambili, ambapo Mhe. Kiganga amepata kura zote 20 kati ya 20 zilizopigwa na wajumbe wa baraza hilo, ikiwa ni ishara ya kuungwa mkono kwa kauli moja.
Ushindi huo wa kishindo ni kielelezo cha imani kubwa waliyonayo madiwani kwa uongozi na maono ya Mhe. Kiganga katika kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wa Geita.
Wajumbe wa baraza wamempongeza kwa ushindi huo na kumtakia mafanikio mema katika kusimamia maendeleo ya Manispaa kwa ushirikiano, uwazi na uwajibikaji.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa