Tarehe 2 Desemba 2025, Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita limeendelea kuonesha mshikamano na umoja baada ya kumchagua Diwani wa Kata ya Nyanguku, Mhe. Elias Charles Ngole, kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani, Mhe. Ngole amepata kura zote 20 kati ya 20 zilizopigwa na wajumbe wa baraza, jambo linaloonesha imani kubwa waliyonayo kwake katika kuendeleza ajenda za maendeleo kwa ushirikiano na Meya pamoja na uongozi wa Manispaa.
Mhe. Ngole ameahidi kushirikiana kwa karibu na viongozi wenzake katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha ustawi wa jamii ya Geita unaimarika.
Wajumbe wa baraza wamempongeza kwa ushindi huo na kumtakia kila la heri katika kutimiza majukumu yake mapya kwa weledi na uadilifu.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa