Mnamo tarehe 11.09.2025, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Dkt. Omari Sukari, akiambatana na timu ya usimamizi wa huduma za afya ngazi ya mkoa, alifanya kikao na timu ya usimamizi wa huduma za afya ngazi ya Halmashauri ya Manispaa ya Geita pamoja na waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya.
Katika kikao hicho, Dkt. Sukari alisisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa huduma za afya, utoaji wa huduma za chanjo, uboreshaji wa takwimu, na ulipaji wa madeni ya dawa kutoka MSD. Pia aliwakumbusha wahusika kuhakikisha kwamba vituo vya afya vinakusanya mapato ipasavyo na kutumia fedha hizo kwa kufuata mwongozo na bajeti iliyopangwa.
Aidha, aliwapongeza waganga wafawidhi wa vituo vilivyofanya vizuri kwa kuhakikisha havina madeni MSD na kwa kukusanya mapato kwa ufanisi. Aliwataka wengine kuiga mfano huo ili kuhakikisha huduma za afya katika Manispaa ya Geita zinaendelea kuimarika na kuwafikia wananchi kwa ufanisi zaidi.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa