Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bomba Mbili – Geita Mjini, yamehitimishwa kwa mafanikio makubwa, yakionesha mchango mkubwa wa sekta ya madini katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Geita na Taifa kwa ujumla.
Akifunga rasmi maonesho hayo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa ndani ya kipindi cha miaka miwili, mahitaji ya umeme mkoani Geita yameongezeka kutoka Megawati 35 hadi 75 ongezeko linalochangiwa na shughuli za wachimbaji wadogo, ambao ni sehemu muhimu ya sekta hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martine Shigela, ameeleza kuwa zaidi ya leseni 9,000 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo, jambo linaloashiria ukuaji mkubwa wa sekta ya madini na kuimarika kwa ushiriki wa wananchi katika shughuli za kiuchumi.
Washiriki na wadhamini wa maonesho hayo wameonesha kuridhishwa na mafanikio ya mwaka huu, huku wakisisitiza dhamira ya kuendelea kushiriki na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuendeleza sekta ya madini nchini.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa