Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeanza rasmi zoezi la usambazaji wa mbegu za viazi lishe katika shule 41 za msingi na sekondari ndani ya manispaa hiyo. Zoezi hili linafanyika kwa lengo la kuimarisha lishe ya wanafunzi kupitia kilimo cha bustani na mashamba yanayomilikiwa na shule husika.
Mbegu zinazotolewa ni za aina ya Kabode, Jewel, Irene na Kakamega, ambazo zinatambulika kwa kuwa na virutubisho muhimu kama vile vitamini A, madini ya chuma na nyuzinyuzi, vinavyosaidia katika ukuaji wa mwili na kuimarisha kinga ya mwili.
Mpango huu unatekelezwa kama sehemu ya afua za lishe na mpango wa chakula shuleni, kwa lengo la kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata angalau mlo mmoja wenye virutubisho anapokuwa shuleni. Hili linaenda sambamba na azma ya serikali ya kuboresha mazingira ya ujifunzaji na kupunguza changamoto za kiafya zinazotokana na lishe duni kwa watoto wa shule.
Zoezi hili linafanikishwa kupitia ushirikiano wa karibu baina ya idara za Afya, Kilimo na Elimu (Msingi na Sekondari), jambo linaloonesha nguvu ya mshikamano wa kiutendaji katika kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma bora na endelevu ya chakula shuleni.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa