Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeendelea kung’ara baada ya kutunukiwa Tuzo ya Mshindi wa Pili katika kipengele cha Halmashauri kwenye Maonesho ya Nane ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Mkoani Geita.
Tuzo hiyo ya heshima imetolewa tarehe 27 Septemba 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahamed Said, katika ukumbi wa Mkapa, uliopo katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tuzo hiyo ni kielelezo cha jitihada na ushiriki wa hali ya juu wa Manispaa ya Geita katika kuendeleza sekta ya madini, teknolojia, na ushirikiano wa karibu kati ya serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa