Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeandaa mafunzo maalum kwa wasanii na wadau wa sanaa, hususan muziki wa kizazi kipya, yaliyofanyika tarehe 26 Septemba 2025.
Mafunzo haya yalitolewa na Abel Phillip Ndaga, Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), akiambatana na baadhi ya maafisa utamaduni na michezo kutoka Manispaa ya Geita.
Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwaelimisha wasanii na wadau wa sanaa kuhusu umuhimu wa kujisajili katika mfumo wa AMIS (Artist Management Information System), mfumo unaowezesha usimamizi bora wa shughuli za sanaa nchini.
Wasanii na wadau wamejitokeza kwa wingi kushiriki mafunzo haya na kueleza kufurahishwa kwao na elimu waliyoipata, huku wakiahidi kuitumia kikamilifu katika kuimarisha kazi zao na kuhakikisha wanajisimamia kitaaluma.
Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za serikali katika kuhamasisha usajili rasmi wa wasanii, kukuza taaluma ya sanaa, na kuwezesha wasanii kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa kupitia mifumo rasmi ya kitaifa.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa