Leo tarehe 9 Septemba 2025 zimefanyika sherehe za kuhitimu kwa wanafunzi wa Jeshi la Akiba kundi la 14/25, waliohitimisha mafunzo yao kwa mafanikio. Jumla ya wanafunzi 308 wamehitimu, wakiwemo wanaume 247 na wanawake 61. Maafali hayo yamefanyika katika viwanja vya Nyanza, Manispaa ya Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba, ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewapongeza vijana hao kwa ukakamavu na uzalendo wao. Amehimiza waendelee kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa kuilinda amani, kupambana na matumizi ya dawa za kulevya, na kusaidia jitihada za serikali katika kuleta maendeleo. Aidha, ameahidi kuwa serikali kupitia sekta mbalimbali itaendelea kulitumia jeshi hilo, ikiwa ni pamoja na kuwajengea fursa za ajira.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Ndugu Yefred Myenzi, ameeleza kufurahishwa na mafunzo na nidhamu waliyoionyesha vijana hao. Amesema kuwa halmashauri inajipanga kuajiri vijana wawili kutoka katika kundi hilo kama sehemu ya kutambua mchango wao.
Sherehe hizo zimefanyika kwa mafanikio makubwa, zikiwa ni ishara ya kuenzi uzalendo na kuandaa vijana kwa ajili ya kulisaidia Taifa katika ujenzi wa maendeleo endelevu.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa