Leo Tarehe 16 Oktoba 2025, Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeadhimisha kilele cha Juma la Elimu la Watu Wazima, Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, na Elimu Jumuishi kwa mafanikio makubwa yanayoonesha dhamira ya dhati ya kuwafikia wananchi wote bila ubaguzi.
Katika kipindi cha mwaka mmoja, Manispaa imefanikiwa kuwasaidia wanafunzi 164 waliokosa nafasi ya kusoma kupitia mfumo rasmi, na kuwawezesha kujiunga na masomo ya sekondari na kidato cha tano.
Aidha, kwa mwaka 2025 pekee, wanafunzi 292 wameingizwa katika mfumo rasmi wa elimu kupitia mpango wa MEMKWA, unaolenga kutoa fursa kwa watoto waliokosa elimu ya awali. Hadi sasa, Manispaa ina vituo 8 vya MEMKWA vyenye wanafunzi 165 wavulana 58 na wasichana 106.
Jamii nayo haijaachwa nyuma. Kupitia mpango wa MUKEJA, wananchi wanapata mafunzo ya stadi za maisha, ikiwemo kilimo, ufugaji, na kusoma, kupitia vikundi vya pamoja vinavyowawezesha kujitegemea kiuchumi.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Bi. Janeth Mobe Afisa Tawala kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika elimu jumuishi na ile nje ya mfumo rasmi ili kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma katika safari ya maendeleo.
Sherehe hizo ni ushahidi wa jitihada za Manispaa ya Geita katika kuhakikisha elimu inapatikana kwa wote, bila kujali changamoto za awali.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa