Tarehe 20 Novemba, 2025 Idara ya Maendeleo ya Jamii imefanya kikao cha tathimini ya usajili wa vikundi vya kijamii huduma ndogo za fedha katika ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita.
Kikao hicho kimeudhuriwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii wote wa Manispaa ya Geita waliopo Makao Makuu na ya Manispaa na wale waliopo ngazi ya Kata.
Katika kikao hicho mikakati ya kuongeza usajili imewekwa kama kufanya kikao na Kamati za Maendeleo za Kata, kukutana na Wawezeshaji wa vikundi pamoja na kufanya mikutano ya kijamii ili kuongeza usajili na kufikia kuvisajili vikundi 250 kwa mwaka.
Katika kikao hicho Benki ya Equity ilitoa mafunzo mafupi ya huduma za kifedha pamoja na huduma za kibenki wanazotoa aidha watafanya kazi na Maafisa Maendeleo ngazi ya Kata katika kutoa elimu ya kifedha kwa vikundi pamoja na kutoa mikopo kwa vikundi vitakavyokidhi vigezo.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa