Leo, tarehe 29 Novemba 2025, Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeendelea na kampeni ya usafi wa mazingira kupitia kampeni ya “HIYAGULAGA GEITA”, kauli mbiu yenye maana ya Safisha Geita. Kampeni hii inalenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kulinda mazingira, kuimarisha afya ya jamii na kuboresha mandhari ya mji.
Zoezi hilo limehusisha ushiriki mpana wa wananchi wa Geita, watumishi wa umma pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, ambao kwa pamoja wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika kusafisha maeneo mbalimbali ya Manispaa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Ndugu Edward Ryoba Mwita — kaimu mkuu wa kitengo cha usimamizi wa taka na mazingira — amewapongeza wananchi kwa moyo wa uzalendo na ushirikiano waliouonesha katika kuhakikisha Geita inakuwa safi na salama.
“Usafi wa mazingira una faida kubwa kiafya, kimaendeleo na kiutalii. Tunashukuru wananchi kwa kuitikia wito huu. Tunaomba kila mmoja awe balozi wa usafi, siyo leo tu bali kila siku, hususan kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi,” amesema Ryoba.
Kupitia kampeni ya HIYAGULAGA GEITA, Manispaa inalenga kuijenga Geita mpya — yenye mji ulio safi, wenye afya na unaovutia kwa uwekezaji na ustawi wa wakazi wake.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa