Leo, tarehe 15 Septemba, Halmashauri ya Manispaa ya Geita imepokea wageni kutoka Access Bank Tanzania, waliowasili kwa lengo la kujitambulisha rasmi na kujifunza fursa mbalimbali za uwekezaji ndani ya manispaa hiyo.
Ugeni huo ulipokelewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Ndugu Yefred Myenzi, ambapo walifanya mazungumzo mafupi yenye lengo la kujadili maeneo yenye nafasi kubwa za uwekezaji kwa taasisi kama Access Bank.
Katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi Myenzi alieleza kuwa manispaa ya Geita ina fursa nyingi zenye kuvutia kwa wawekezaji, ikiwemo sekta za uchimbaji wa madini, elimu, afya, biashara pamoja na huduma za kifedha, akisisitiza kuwa Halmashauri iko wazi kwa taasisi yoyote yenye dhamira ya kuleta maendeleo kupitia uwekezaji endelevu.
Wageni kutoka Access Bank walitoa shukrani za dhati kwa mapokezi mazuri na kwa kupewa taarifa za kina kuhusu fursa zilizopo. Wameonesha nia ya dhati ya kuendelea kufuatilia maeneo hayo kwa ajili ya kushirikiana na Halmashauri katika kuendeleza uchumi wa eneo hilo na kuinua maisha ya wananchi kupitia huduma bora za kibenki na uwekezaji wa kijamii.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa